PAZA yawanufaisha wanawake zaidi ya 100 Kusini Unguja

Elimu ya Mradi wa kukuza uwajibikaji Zanzibar PAZA ulioundwa na TAMWA kwa kushirikiana na WAHAMAZA na NGENARECO uliohusisha Wilaya tofauti Zanzibar  Wanawake zaidi ya 100 wa Mkoa wa Kusini Unguja waliopewa elimu ya kujua haki zao wamesema elimu waliopewa imewasaidia sana katika kujua haki zao na kufanikiwa kuzidai katika mamlaka zinazohusika.

Hayo yameelezwa hivi karibuni na wajumbe wa mitandao ya kupambana na udhalilishaji katika vijiji mbali mbali ikiwemo Muunguno, Kitogani na Bwejuu wilaya ya kusini Unguja wakati wa kufanyika tahmini ya Mradi wa Kukuza Uwajibikaji Zanzibar (PAZA).

Wanawake hao wamesema wamehamasikia na elimu ya kukuza Ujibikaji  Zanzibar kupitia asasi za kirai na mitandao ya ardhi ambapo elimu hiyo imewaleta maendeleo katika maakazi yao ikiwemo kuondokewa na tatizo la maji, afya na elimu.

Mkaazi wa Kitogani Bwana Hajji Iddi Hassan (25) amesema miradi kama hii ya maendeleo inayokuja kwenye vijiji vyao husaidia kwa kiasi kikubwa kuwachangamsha vijana na wazee katika maeneo hayo kwa kuwa mbali na kupata elimu lakini inawapa ujasiri wa kuweza kueleza matatizo yao hata mbele ya viongozi.

Bwana Hajji amesema jambo hilo ni zuri na linapasw akuendelezwa hata kama Mradi utakuwa umemaliza muda wake lakini bado wanaharakati wana nafasi ya kuendelea kuwapa elimu wana kijiji ili waweze kujitambua na kudai haki zao katika maeneo yao kwani changamoto zilizopo ni nyingi na zinapaswa kutatuliwa na viongozi wenye mamlaka.

“Mimi ombi langu kwenu kuwa naomba watendaji wa Mradi wa PAZA kuendeleea na mradi kwa sababu bado watu wanamuamko mdogo wa kuhudhuri mkutano lakini kila mnavyokuja wanawake na vijana wananufaika na wanajitokeza kwa ajili ya kupata elimu” alisema.

Akizungumza na muandihi wa habri hizi Mwana asasi za kiraia Halda Nassor Haji (32) amesema  amewahamasisha wanawake 100 elimu ya kukuza uwajibishaji katika shehia hizo ili waondokane matatizo katika maeneo hayo.

Amesema wanaasasi wote walipewa mafuzo na chama cha waandishi wa habari wanawake Zanzibar (TAMWA-Zanzibar) kupitia Mradi wa Kukuza uwajibikaji Zanzibar (PAZA) na kuwataka elimu hiyo kuwafikishia wanawake wenzao vijijini.

Halda amesema wametumia njia ya mkutano kuwaeleza elimu hiyo akinamama ambapo pia kila mwanakijiji alipata fursa ya kuibua matatizo yalimkabili katika eneo lake.

Wahida Khatib Mkaazi wa Maungoni kwa upande wake akizungumzia mradi huo amesema yeye ni miongoni mwa wanawake walionufaika kupitia mradi wa PAZA ambapo amesema hivi sasa wanawake wa vijiji vyao wanaweza kusimama na kuongea lakini pia namna ya kwenda kudai haki kwenye halmashauri.

 “Paza imenielimsha naweza kuandika barua ya malalamiko ya shida ya maji na kupeleka Halmashauri na kufuatilia hadi kufikia hatua ya mafanikio, tulihudhuria mkutano sisi wote tuwaweza kutatua matatizo yetu kwa sasa”  Amesema Wahida.

Amesema ameridhika kwa kiwango cha juu, Mradi wa PAZA umewaondolea matatizo mengi, wilaya ya kusini ikiwemo tatizo la utoro kwa wanafunzi, shida ya mji safi na salama, ukarabati wa vitua vya afya na majengo ya skuli ambapo sasa hivi viongozi wa serikali za mitaa wamekuwa wakishughulikia matatizo ya wananchi.

“Viongozi wetu wa serikali za mitaa wanashughulikia matatizo yetu na sisi tunawakera kwa kwenda kuwadai angalau kidogo shida zetu tunajua pa kuzipeleka” ameongeza.