Picha: Angalia namna Miji ilivyo shangiria sherehe za Mwaka Mpya wa 2019

Shangwe, vifijo, nderemo zilisheheni miji mbalimbali watu wakisherehekea kuanza kwa Mwaka Mpya wa 2019 katika majiji mbalimbali duniani, fataki nazo zikatanda angani.

Fataki hapa zinaonekana London Eye ambapo zilirushwa angani kwa dakika 10 hivi katikati mwa London
Image captionFataki hapa zinaonekana London Eye ambapo zilirushwa angani kwa dakika 10 hivi katikati mwa London
"Yellow Vest", waandamanaji wanaovalia fulana za rangi ya manjano nchini Ufaransa walikuwa miongoni mwa waliokuwa wanaandamana karibu na Champs-Elysees jijini Paris
Image caption”Yellow Vest”, waandamanaji wanaovalia fulana za rangi ya manjano nchini Ufaransa walikuwa miongoni mwa waliokuwa wanaandamana karibu na Champs-Elysees jijini Paris
Hapa, fataki zinaonekana juu ya sanamu ya Quadriga katika lango maarufu la Brandenburg Gate, Berlin
Image captionHapa, fataki zinaonekana juu ya sanamu ya Quadriga katika lango maarufu la Brandenburg Gate, Berlin
Wanandoa hawa nao wanaonekana wakikoleza upendo wao kama sehemu ya sherehe za kuulaki Mwaka Mpya eneo la Red Square, Moscow
Image captionWanandoa hawa nao wanaonekana wakikoleza upendo wao kama sehemu ya sherehe za kuulaki Mwaka Mpya eneo la Red Square, Moscow
Jijini Nairobi, fataki zinaonekana zikirushwa angani wakati wa sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya
Image captionJijini Nairobi, fataki zinaonekana zikirushwa angani wakati wa sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya
Na hapa, mwanaulimbwende anaonekana akipamba nywele ya mmoja wa watu waliojitokeza mjini Ahmedabad, India kwa sherehe za kuulaki mwaka mpya
Image captionNa hapa, mwanaulimbwende anaonekana akipamba nywele ya mmoja wa watu waliojitokeza mjini Ahmedabad, India kwa sherehe za kuulaki mwaka mpya
Maelfu walikusanyika pia Pyongyang, Korea Kaskazini kwa maonesho ya fataki katika uwanja wa Kim Il Sung
Image captionMaelfu walikusanyika pia Pyongyang, Korea Kaskazini kwa maonesho ya fataki katika uwanja wa Kim Il Sung
Hapa ni fataki zikirushwa na watu ufukweni Gangneung, katika mkoa wa Ganwon, Korea Kusini
Image captionHapa ni fataki zikirushwa na watu ufukweni Gangneung, katika mkoa wa Ganwon, Korea Kusini
Katika jengo refu zaidi duniani, Burj Khalifa, Dubai, fataki zilikuwa tele pia
Image captionKatika jengo refu zaidi duniani, Burj Khalifa, Dubai, fataki zilikuwa tele pia
Ufilipino, huyu aliamua kuvalia miwani ya 'kumsaidia kuuona vyema' Mwaka 2019 katika sherehe iliyofanyika katika eneo la Metro Manila, jijini Quezon
Image captionUfilipino, huyu aliamua kuvalia miwani ya ‘kumsaidia kuuona vyema’ Mwaka 2019 katika sherehe iliyofanyika katika eneo la Metro Manila, jijini Quezon
Waumini wa Kibuddha nao hapa wanaonekana wakiwasha mishumaa kuukaribisha Mwaka wa Nguruwe kwa mujibu ya miaka ya nyota ya Kichina katika hekalu la Jogyesa jijini Seoul, Korea Kusini
Image captionWaumini wa Kibuddha nao hapa wanaonekana wakiwasha mishumaa kuukaribisha Mwaka wa Nguruwe kwa mujibu ya miaka ya nyota ya Kichina katika hekalu la Jogyesa jijini Seoul, Korea Kusini
Hapa watu wanaonekana wakijaribu kupiga picha fataki zilizorushwa kwenye jengo refu maarufu la Taipei 101 nchini Taiwan
Image captionHapa watu wanaonekana wakijaribu kupiga picha fataki zilizorushwa kwenye jengo refu maarufu la Taipei 101 nchini Taiwan
Anga ya Hong Kong pia ilipambwa kwa fataki watu wakiukaribisha mwaka 2019 nchini China
Image captionAnga ya Hong Kong pia ilipambwa kwa fataki watu wakiukaribisha mwaka 2019 nchini China
Sherehe ya Mwaka Mpya pia ilifanyika Beijing, China
Image captionSherehe ya Mwaka Mpya pia ilifanyika Beijing, China
Na Marina Bay, Singapore kulikuwepo uhondo zaidi
Image captionNa Marina Bay, Singapore kulikuwepo uhondo zaidi
Huko Sydney Harbour Bridge nchini Australia, maonyesho ya fataki yalidumu dakika 12
Image captionHuko Sydney Harbour Bridge nchini Australia, maonyesho ya fataki yalidumu dakika 12.