MKUU wa Mkoa wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa Habari, uwanja wa michezo Gombani Pemba, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Malaria duniani, (Picha na Haji Nassor, Pemba)

 

MTANGAAZAJI wa ZBC redio kisiwani Pemba, Khadjia Kombo Khamis, akichangia jambo, kwenye mkutano wao, ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Malaria duniani, yaliofanyika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba, ambapo Kitengo cha Malaria kisiwani Pemba, kimeaadhimisha siku hiyo, kwa kuzungumza na vyombo vya habari, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 

WAANDISHI wa Habari wa vyombo mbali mbali kisiwani Pemba, wakifuatilia hutuba ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla, akizungumza nao kwenye maadhimisho ya siku ya Malaria duniani, yaliofanyika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 

WATENDAJI wa kitengo cha Malaria kisiwani Pemba pamoja na waandishi wa habari, wakilisukuma gari la Kitengo cha Malaria, kwenye uwanja wa michezo Gombani, mara baada ya kuamalizika maadhimisho ya siku ya malaria dunia, ambapo kwa Pemba yalifanyika mjini Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).