Picha: Yaliyojiri ziara ya Waziri wa afya Zanzibar katika Hospitali ya Makunduchi

Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed kulia akifanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja kuangalia Miradi na mafanikio mbalimbali yanayo patikana katika hospitali hiyo.

 

Daktari wa Hospitali ya Makunduchi Vuai Abdalla (MD) akimuelezea Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed maendeleo na changamoto zinazowakabili katika Hospitali hiyo.

 

Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akisalimiana na Mzazi Asia Issa Hassan mkaazi wa Makunduchi aliyekuja kujifungua katika Hospitali hiyo na kumuelezea furaha yake ya kufuata uzazi wa Mpango.

 

Muonekano wa Jengo jipya la kituo cha Watoto liliopo ndani ya Hospitali ya Makunduchi.

 

Muonekano wa Jengo litakalotumika kama Makaazi ya Madaktari kwa ajili ya kuondoa usumbufu wa Madaktari waliokuwa hawana nyumba ya kuishi katika Hospitali hiyo.

 

Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akimsikiliza Mpishi wa kituo hicho Suleiman Mohammed Suleiman aliyekuwa akimuelezea changamoto wanazokabiliana nazo katika kutoa huduma ya chakula.

Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar.