Katibu wa NEC – Itikadi na Uenezi – CCM Ndg. Humphrey Polepole amewaonya walichaguliwa umeya kutokufaya sherehe baada ya kuchaguliwa nafasi hizo.

“Hawa ninaowataja leo hamtakiwi kusheherekea, kipindi hiki hatutokuwa na mzaha kwa viongozi ambao watashindwa kuwajibika katika kushughulika na utatuzi wa kero za watu wetu, mnafahamu tuna kama siku elfu moja na mia nane na ishirini na tano hivi ndio tunazo sababu nikisema miaka mitano mnaweza kuona ni mingi sana” – Ndg. Humphrey Polepole, Katibu wa NEC – Itikadi na Uenezi – CCM.