Polis jamii apigwa mapanga kichwani akiwa Doria

Askari jamii katika Mtaa wa Kirika B kata ya Osunyai Jijini Arusha amepigwa Panga sehemu za kichwana wakati akiwa kwenye Doria na vijana watatu ambao waliwavamia usiku na kutokomea kusikojulikana.

Akizungumza Askari jamii huyo John Mussa ambaye amepatwa na adha hiyo amesema kuwa wakati wakiwa katika lindo ilitokea pikipiki ambayo hawakuielewa ikiwa imebeba vijana watatu walivyowasimamisha ili wajue ni wakina nani waliamua kumkata na panga kichwani ambapo ameshonwa Nyuzi kumi baada ya kukimbizwa hospitali.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo ambaye anasimamia masuala ya ulinzi na usalama Christopher Rutagerera amesema kuwa jambo hilo limemsikitisha kwa kuwa askari jamii hao wanaonyesha uzalendo wa kuhakikisha mtaa unakaa salama lakini bado wanakabiliana na uhalifu nyakati za usiku na kuahidi kwamba watashiriana kubaini wahalifu hao.

Nao baadhi ya Askari jamii waliokuwepo wakati tukio hilo linatokea wamesema kuwa licha ya kwamba mambo hayo yanajitokeza lakini hawatakata taama kwa kuwa wameamua kufanya mtaa huo kubaki salama bila kuwepo na vitendo vya wizi nyakati za usiku.