Jeshi la polisi Mkoa wa Mjini Magharib limetoa onyo kali na tahadhari kwa wale wote wanatumia vibaya mitandao ya kijamii kwa kupotosha na kusambaza taarifa za uongo kuhusu ugonjwa wa corona

hayo yamesemwa na Kamanda wa jeshi la polisi wa mkoa huo ACP Awadhi Juma Haji wakati akizungumza na waandishi wa habari huko katika ofisi zake Madema Mjini Zanzibar

Amesema uzushi huo unaleta hofu na taharuki kwa wananchi jambo ambalo ni kosa kwa mujibu wa sheria

Aidha kamanda amewaonya wafanya biashara wanaotumia fursa ya janga hili la ugonjwa wa CORONA kupandisha bei za bidhaa na kufanya wananchi kuwa na hali ngumu hivyo atakaebainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu yake