Kwa mara ya kwanza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa posti ya kwanza mitandaoni tangu anusurike kwenye ajali mbaya ya gari wiki iliyopita.

Kigwangalla kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa usiku wa kuamkia leo kitu Cha kwanza alichongaa ni kushika simu yake ya mkononi. Jambo ambalo limemfanya aumie sana baada ya kukutana na picha za aliyekuwa Mwandishi wa Wizara yake, Hamza Temba ambaye alifariki kwenye ajali hiyo iliyotokea wiki iliyopita.

Mwandishi wa Habari Hamza Temba ni moja ya watu waliyokuwemo kwenye ajali hiyo iliyotokea mkoani Manyara wakati Waziri Kigwangalla akiwa kwenye majukumu yake.