Prince Harry ametangazwa kuwa Mshindi wa Peoples Magazine kwenye kipengele cha Mwana-Mfalme mwenye mvuto zaidi Duniani ambaye bado anaishi akiwashinda wenzake kibao akiwemo Kaka yake Prince William.

Mshiriki ambaye alikuwa anamkaribia na alikuwa Mpinzani wake wa karibu ni Prince Carl Philiph (41) kutoka Nchini Sweden.

Harry anashinda nafasi hii ukiwa umepita mwaka mmoja tu tangu alipotangazwa kuwa ni Baba mwenye mvuto zaidi kati ya Mababa wote wenye Watoto Duniani.