Spika Mstaafu wa Bunge  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia , Pius Msekwa, amesema kwa mujibu wa katiba Halima Mdee na wenzake 18, hawana tena sifa za kuwa wabunge kwa kuwa hawana chama kilichowapeleka Bungeni na hata wakihamia chama kingine hawawezi kupata nafasi hizo, labda mpaka uchaguzi ujao.