Mwanamuziki Queen Darleen amefunga ndoa kimya kimya na mfanyabiashara wa magari jijini Dar es salaam.

Muimbaji huyo ambaye yupo chini ya WCB, amefunga ndoa siku ya jana na kuhudhuriwa na ndugu jamaa na marafiki.

Kwa mujibu wa picha ambazo zimesambaa mitandaoni zinadai kwamba mfanyabiashara hiyo anaitwa Isihaka.

“Sijui nilie jana nimekosa ila tunairudia hongera sana ndugu yangu dadaangu Mungu akubariki ktk ndoa yako akuepushe na husda za walimwengi yani daah Mungu ni mwema shem langu nakupenda sina cha kusema Wallah @queendarleen_ jishebedue wakuone 👌 ridhiki mafungu saba,” alindika Esma kupitia Instagram.

Wadau wa mambo wanadai huwenda hiyo isiwe ndoa kwani, kwani mwanaume huyo ambaye ameonekana kwenye picha hapo juu ni mume wa watu.