Queen Darleen awajibu wanaomshambulia kwa kuvaa nusu utupu

Msanii wa muziki nchini Queen Darleen amewajibu wanaomshambulia kuwa anavaa nusu utupu jambo ambalo ni kinyume na maadili ya Mtanzania.

Queen Darleen kupitia mahojiano yake na Wasafi TV amewataka wanaomsema vibaya juu ya mavazi yake wasimpangia maisha wala mavazi.

Kama mimi navaa najiona mwenyewe napendeza, niko fresh, lakini mtu anakuja anakwambia unavyovaa umevaa vibaya hujapendeza? My Friend pesa yangu ambayo nimenunulia nguo mimi unayoniambia sijapendeza, hiyo simu yako uliyoshika gharama yake hazilingani.. Tusipangiane mavazi wala maisha.“amesema Queen Darleeen.

 

Queen Darleen
Kuhusu muziki Queen Darleen ameahidi kuachia kazi yake mpya ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa na amewataka mashabiki wake wawe wavumilivu kwani WCB kuna mfumo wa namna ya kuachia ngoma.