Raia mmoja wa Italy amejeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hospitali ya Mnazimmoja baada ya kushambuliwa na Watu wasiojulikana kwa kupigwa tofali la kichwa huko Matemwe wilaya ya Kaskazini A Unguja.

Taarifa zilizopatikana zinasema kuwa mtu huyo alikuwa Nyumbani kwake majira ya saa 10 Usiku ndipo walipotokea watu hao na kumshambulia.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo la kusikitisha Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Unguja Haji Abdalla Haji, amesema wamepokea taarifa hizo leo majira ya saa 10 usiku na teari jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kuwabaini waliohusika na tukio hilo.

Hadi sasa Majeruhi anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Mnazimmoja na hali yake  inaendelea vizuri.