Mwanamume mmoja raia wa Uingereza anayetuhumiwa kwa kupora bunduki ya afisa mmoja wa polisi katika mkutano wa kisaiasa wa Donald Trump, amewaambia wapelelezi wa Marekani kuwa, alitaka kumuua kwa kumpiga risasi na kumuuwa mgombea huyo wa kiti cha Urais wa chama cha Republican.

Kwa mjibu wa stakabadhi za mahakama, Michael Sandford anasema kuwa aliendesha gari hadi Las Vegas akiwa na nia ya kumpiga risasi Bw Trump siku ya Jumamosi.Awali Donald Trump alimtimua Maneja wake wa kampeni Corey Lewandowski kwa kutofautana naye katika kauli zake.

Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden amemlaum Trump kwamba kauli zake ni za hatari