Kiongozi mkuu wa ngome ya upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ametangaza kutokushiriki tena katika chaguzi za kuwania urais Kenya mwaka 2022.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumatatu na msemaji wake, Dennis Onyango, Odinga amesema atajikita katika kujenga miundombinu katika bara la Afrika pamoja na kuwaunganisha Wakenya ikiwa ni moja ya majukumu yake aliyopewa na Tume ya Umoja wa Afrika.

“Bw. Odinga anapenda kuwataarifu kuwa hatajihusisha na siasa za kurithishana madaraka kuelekea uchaguzi mkuu wa 2022,” taarifa hiyo inasomeka.

“Odinga anataka kutumia miaka kadhaa ijayo kujikita katika kujenga miundombinu barani Afrika kupitia ofisi yake mpya pamoja na kuhakikisha anajenga daraja la kuwaunganisha Wakenya, kupitia kampeni ya ‘Kujenga Daraja Kuelekea Taifa Jipya la Kenya (BBI)’,” ameongeza.