Rais John Magufuli ameongeza siku 20 kuanzia Januari 1, 2020 kwa watu wote watakaoshindwa kusajili laini zao za simu kwa alama za vidole ifikapo Desemba 31

Desemba 31 ulikuwa ndiyo ukomo wa muda wa awali wa kuwataka wananchi kusajili laini zao kwa alama za vidole kwa kutumia Kitambulisho cha Taifa (NIDA) ambapo kwa mujibu wa TCRA baada ya hapo laini ambazo zingekuwa hazijasajiliwa zingefungwa

Pamoja na hayo, Rais mwenyewe amesajili laini yake kwa alama za vidole