Obama2

Rais wa Marekani Barack Obama amempiga kijembe Donald Trump anayetarajiwa kukiwakilisha chama cha Republican katika uchaguzi wa rais mwezi Novemba, akisema ‘Ujinga sio sifa nzuri”.

Ingawa Obama hakumtaja moja kwa moja Trump, ilikuwa bayana kuwa alimlenga mgombea mwenye kauli mbiu isemayo, ”Kuifanya Marekani kuwa Maarufu tena”. Rais Obama ambaye alikuwa akizungumza katika mahafali kwenye chuo kikuu jimboni New Jersey, aliwaasa wanafunzi kutong’ang’ania kile kinachoitwa ‘siku zilizopita zenye neema”, akisema sio kila kitu kilikuwa kizuri wakati huo.