RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Tukio hilo limefanyika leo huko katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil, Kikwajuni Jijini Zanzibar ambapo Rais Dk. Mwinyi alisaini kitabu hicho mnamo majira ya saa tatu za asubuhi.

Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad alifariki dunia mnano Februari 17, 2021 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar-es-Salaam na kuzikwa huko kijijini kwao Nyali Mtambwe, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kusini Pemba.