Leo Novemba 8, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa shukurani za dhati kwa taifa la Israel kwa kuiunga mkono Tanzania katika harakati za kimaendeleo.

Rais Magufuli ametoa shukurani hizo Ikulu Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na jopo la Madaktari  wa moyo kutoka nchini Israel na Marekani ambao wanashirikiana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete hapa nchini.

Nimeandika barua ambayo nitakukabidhi Balozi, umpelekee Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu inayoeleza namna ninavyokubali utendaji kazi wake, najua hii barua itamfikia ili kuonesha kazi nzuri mliofanya,” amesema Rais Magufuli.

Ameongeza kuwa “Niwaombe Madaktari na Wataalamu kutoka Israel mkija msije tu kwa masuala  ya Udaktari siku nyingine mnaweza mkaja kwa masuala ya kufurahi,  mnaenda Serengeti National Park, Ngorongoro na maeneo mengine ambayo ni  ya kuvutia“.

Madaktari hao zaidi ya thelathini wamekuja nchini kwaajili ya kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto 51 katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya taifa ya Muhimbili.