Rais Dkt. John Magufuli, leo Oktoba 11, 2018 amemteua Dkt. Dalmas Lucas Nyaoro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Dkt. Dalmas Lucas Nyaoro

Dkt. Nyaoro ambaye ni mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), ana uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika sekta ya uhandisi wa masuala ya Ardhi na teknolojia, (Geotechnical).

Nyaoro ni mbobezi wa masomo ya Hydrogeological akimiliki PhD na MSc katika mitambo ya udongo kutoka Chuo cha Imperial (UK).

Pia ni mhandisi aliyesajiliwa na bodi ya wahandisi nchini, ambaye ni mwanachama wa Taasisi ya wahandisi Tanzania.

Soma taarifa kamili ya uteuzi: