Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Alphaxard Lugola aliyefiwa na Mkewe Mary Lugola.

Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu Kikosi cha Polisi Reli Tanzania.

Mary alifariki dunia jana tarehe 01 Januari 2018 katika hospitali ya Rabinisia Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu na msiba upo Gerezani Railway Club Jijini Dar es Salaam.