Rais John Magufuli amewataka wanawake nchini Tanzania kutofunga vizazi vyao ili kuweza kuzaa watoto wengi kama njia mojawapo ya kupiga jeki uchumi wa taifa hilo kwa ili kuwa taifa lenye uchumi mkubwa Afrika mashariki , hatua ambayo wakosoaji wanasema itasababisha ukosefu wa usawa na kuleta umasikini kulingana na chombo cha habari cha Reuters.

”Wakati unapokuwa na idadi kubwa ya watu unajenga uchumi . Ndio kwa sababu uchumi wa China ni mkubwa” , akitoa mfano wa mataifa kama vile India na Nigeria kama mataifa yalioimarika kiuchumi kutokana na idadi kubwa ya raia.

‘Najua kwamba wale wanaopendelea kufunga vizazi watalalamika. Lakini wekeni huru vizazi vyenu, wawacheni wafunge vyao”, aliambia umati mkubwa wa watu nyumbani kwake huko Chato.

Kulingana na Reuters tangu alipochukua hatamu 2015 , rais Magufuli ameanzisha kampeni ya ujenzi wa viwanda ambao umesaidia ukuwaji wa uchumi wa taifa hilo unaokuwa kwa wastani wa kati ya asilimia 6-7 katika miaka ya hivi karibuni.

Rais John Pombe Magufuli

Lakini anasema kuwa kiwango cha juu cha akina mama wanaojifungua watoto kitasababisha maendeleo ya haraka.

Tanzania ina ukuwaji wa kati ya wastani wa asilimia 6-7 kila mwaka, katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Idadi ya watu kufikia 2015

Wakati huohuo , taifa hilo la Afrika mashariki lenye idadi ya watu milioni 55 lina kiwango cha juu cha watoto wanaozaliwa – huku mwanamke mmoja akidaiwa kuwa na watoto watano.

Kulingana na chombo cha habari cha Reuters, Data kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia idadi ya watu UNFPA inaonyesha kuwa Idadi ya watu nchini Tanzania inakuwa kwa asilimia 2.7 kila mwaka huku hospitali na shule nyingi za Umma zikiripoti idadi kubwa ya watu na vijana wengi hawana ajira.

UNFPA inasema kuwa thuluthi moja ya wanawake walio katika ndoa nchini Tanzania hutumia kinga wakati wa kufanya tendo la ndoa , lakini magufuli amekosoa mipango ya upangaji uzazi ya mataifa ya magharibi inayotekelezwa na wizara ya afya.

Msongamano wa watu Afrika mashariki kufikia 2015