Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli leo amezindua Msikiti mpya wa Chamwino Dodoma ambao August mwaka huu alioongoza kuchangisha michango ya kuujenga.

“Niliendesha Harambee Kanisani Aug 23 mwaka huu na Waumini wengi wakachangia wakiongozwa na Baba Askofu, Paroko na Wakristo wote na baadaye wengine wakajitokeza kutuunga mkono, tukapata Tsh Mil 319.3 ambazo zimetumika kujenga Msikiti huu, nawashukur wote waliochangia”– JPM

“Nawapongeza JKT wamefanya kazi nzuri, niliwaambia kwasababu Msikiti umepewa jija la Mufti pajengwe na kagorofa pale ili hata akija awe analala hapa badala ya Hotelini”– JPM

“Namshukuru Sheikh Mkuu wa Msikiti wa Chamwino, nichango ya ujenzi wa Msikiti ilianzishwa Kanisani bila kumwambia, ila nilipokuja kumkabidhi akakubali namshukru, hii ni dalili za kwamba Nchi yetu haina Dini”– JPM

“Kuna pesa iliyobaki kwenye ujenzi wa Msikiti kama mtanikubalia tuichangie , tulianza na Kanisa wanalosali Jumapili, leo tumekamilisha Msikiti wanaosali Ijumaa, hii iliyobaki ikawe chanzo cha Kanisa wanalosali Jumamosi, na kama nikirudi hapa Chamwino tutaendelea ili Madhehebu yote yawe na sehemu ya kuabudia hapa Chamwino, huwezi kuwa na Ikulu na ukakosa eneo la kuabudia”– JPM