Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu Chama Cha Mapinduzi ikiwepo kukiimarisha wakati wa kwenda kwenye uchaguzi.

Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi CCM na Dkt. Shein ambaye Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar wamezungumzia masuala mbalimbali yanayohusu chama hicho Ikulu jijini Dar es salaam.

Baada ya mazungumzo hayo Dkt. Shein amesema wamejadili kuhusu kuimarisha Chama cha Mapinduzi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu mwaka 2020.

Hata hivyo viongozi hao wamezungumzia masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofanywa kwa ushirikiano wa Japan na Tanzania hususani ujenzi wa barabara na madaraja.