Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Jijini Dar es salaam ambapo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ziara hiyo itaanza kesho siku ya Jumatano Februari 24, 2021 ambapo Rais atazindua Daraja la juu Ubungo (Ubungo interchange) majira ya saa 03:30 asubuhi na Mara baada ya hapo ataelekea Mbezi kwa ajili ya uzinduzi wa Kituo Cha Mabasi yaendayo Mikoani na Nje ya Nchi cha Mbezi Luis .

Siku ya Alhamis ya Februari 25, Rais Dkt. Magufuli ataweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Soko la Kisasa Kisutu majira ya saa 03:30 Asubuhi na baada ya hapo atafanya shughuli ya uzinduzi wa Jengo la Jitegemee House,

Hata hivyo Rais Magufuli atahitimisha Ziara yake Siku ya Ijumaa ya Februari 26 ambapo atafanya shughuli ya uzinduzi wa Nyumba za Jeshi la Polisi na Kiwanda Cha kutengeneza sare za Askari Polisi.