97

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin mara baada ya kuombewa dua yeye pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

98

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimshukuru Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin mara baada ya kuombewa dua yeye pamoja na Rais Dkt. Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

101

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea mfano wa moja ya Hundi ya USD (100,000) kutoka kwa kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin aliyechangia jumla ya kiasi cha dola za Kimarekani 250,000/- kwa ajili ya waathirika wa Maafa ya Tetemeko lililotokea mkoani Kagera.

103

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika mazungumzo na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

96

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfafanulia jambo Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin wakati wakitazama Taaswira ya Simba Ikulu jijini Dar es Salaam.

95

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.