Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 9(1) cha Sheria ya Kikosi cha Valantia Namba 5 ya 2004, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Major Said Ali Juma Shamhuna kuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia (KVZ) Zanzibar.

Major Said Ali Juma Shamhuna anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Kikosi hicho Lt. Col. Mohamed Mwinjuma Kombo ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee uteuzi huo unaanzia tarehe 13 Juni 2019.