Rais wa jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi ametangaza hali ya dharura na kufunga mipaka baada ya maambukizi ya Covid_19 kuendelea kuongezeka. Pia, ametangaza kusitisha safari za ndani na nje ya Mji Mkuu wa nchi hiyo, Kinshasa

Ikumbukwe kuwa Siku ya Jumatatu Machi 23, Mji wa Lubumbashi ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini humo ulifungwa kwa saa 48 baada ya watu wawili kupatikana na maambukizi ya Virusi vya Corona

Hadi sasa, idadi ya maambukizi ya COVID_19 iliyoripotiwa nchini humo ni 48 na watu watatu wamefariki dunia