Rais wa Botswana, Mokgweetsi Eric Masisi atakuwa Karantini kwa siku 14 baada ya kurudi nchini humo akitokea Namibia ambapo watu watatu wamethibitishwa kuwa na maambukizi ya Coronavirus

Rais Masisi alienda Namibia kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo, Hage Geingob. Viongozi wengine waliokuwepo ni pamoja na Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe na Rais Joao Lourenco wa Angola

Taarifa ya Serikali imesema Rais Masisi atapimwa ili kufahamu kama ameambukizwa COVID_19, na atakuwa mbali na familia yake muda wote wa Karantini. Waliokuwa na Rais huyo pia wametengwa na watapimwa