Ikiwa ni miezi minne kabla ya Uchaguzi wa Urais Burundi, ambao Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesema hatawania, Bunge la nchi hiyo limepitisha Sheria inatakayompa Rais Nkurunziza dola 500000 sawa na Tsh Bilioni 1.15 atakapostaafu. Upinzani umelalama kuwa fedha hizo ni nyingi mno

Pia, Bunge la Burundi limepitisha Muswada wa Sheria unaompa Rais Pierre Nkurunziza cheo cha Kiongozi Mkuu. Sheria hiyo iliyotetewa Bungeni na Waziri wa Sheria Aime Laurentine Kanyana, inaagiza pia Rais atakapostaafu kuchukuliwa kwa Hadhi ya Makamu wa Rais kwa kipindi cha miaka 7

Muswada huo pia utamuwezesha kulipwa mshahara kwa kipindi chote cha maisha yake, kupata marupurupu yote anayopewa Makamu wa Rais aliyeko madarakani na atapewa nyumba ya kifahari, anayopewa kila Rais wa Burundi