Rais wa Malawi Peter Mutharika amechukua uongozi wa asilimi 40.44 ya kura zote zilizopigwa katika uchaguzi mkuu wa mwezi Mei huku ikiwa asilimia 75 ya kura hizo zimehesabiwa kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo..

Lazarus Chakwera , ambaye anaongoza chama pinzani cha Malawi Congress Party amejipatia asilimia 35.34 huku makamu wa rais Saulos Chilima amejipatia asilimia 18.35, tume hiyo iliambia mkutano na wanahabari.

Mapema Alhamisi kiongozi wa upinzani nchini Malawi Lazarus Chakwera alichukua uongozi wa mapema baada ya chama chake cha MCP kujipatia kura 533,217 ambayo ni sawa na asilimia 37.65.

Alikuwa annafuatiwa kwa karibu na rais Peter Mutharika ambaye aalikuwa amejipatia kura 524,247 ikiwa ni asilimia 37.1 huku makamu wa rais Saulos Chilima wa United Transformation Movement akiwa wa tatu na kura 293,978 ambayo ni asilimia 20.76.

Lazarus Chakwera alisema kuwa matokeo hayo ya mapema yalimpatia uongozi katika uchaguzi huo.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mapema Jumanne

Hatahivyo aliongezea kwamba kulikuwa na jaribio la baadhi ya watu wasiojulikana kuingilia matokeo ya uchaguzi huo huku akiapa kwamba hatokubali udanganyifu wowote.

Lakini tume ya uchaguzi nchini humo imetoa wito wa kuwepo kwa utulivu ikisisitiza kuwa ndio yenye uwezo wa kutangaza matokeo hayo.

Uchaguzi huo umekumbwa na ushindani wa karibu kati ya rais Peter Mutharika , makamu wake Saulos Chilima na Chakwera ambaye anakiongoza chama cha Malawi Congress party.

Katika uchaguzi wa 2014 , Chakwera alipoteza kwa karibu dhidi ya rais Mutharika na akashindwa kupinga uchaguzi huo mahakamani.

Tume ya uchaguzi ina hadi siku nane kutangaza matokeo hayo .

Hatahivyo imekiri kwamba inakabiliwa na changamoto za kiufundi katika utangazji wa matokeo hayo.

Hatahivyo inasema kuwa ina imani kwamba itatoa matokeo yalio huru na haki.

Takriban raia milioni 6.8 wa Malawi walisajiliwa kushiriki katika uchaguzi huo kumchagua rais mpya , mbunge mpya na madiwani.

Inadhaniwa makamu wa rais Saulos Chilima ana umaarufu mkubwa miongoni mwa wapiga kura vijana nchini