“Nilipiga simu juzi kumuuliza Rais Magufuli uko wapi, na mara nyingi tunaongea asubuhi mapema, akasema yupo Chato, nikamuuliza Chato ni wapi? akasema Chato nyumbani, nikamwambia nakuja kuona kwenu, shule uliyosoma, akasema njoo, nikamwambia sili sembe nakula ugali wa kusaga akasema nitakusagia”-Filipe Nyusi,Rais wa Msumbiji

“Nakupongeza Rais Magufuli kwa kujenga Hospitali hii ya Rufaa ya Kanda ya Chato, Hospitali hii haina Chama itatumiwa na wote, nashukuru kwa kunipa heshima ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali hii, nitakuwa napiga simu kila Jumamosi kuulizia ujenzi umefikia wapi”-NYUSI

“Wakati najiandaa na Kampeni za Urais nilikuja Tanzania, Mama Maria Nyerere alinipokea akanipikia mbuzi nyumbani kwake, akaniambia ukiwa Rais, ukishindwa vingi angalau ujenge kiwanda kimoja cha dawa, kwahiyo nakupongeza JPM, kwa kushughulika na afya za Wananchi, afya muhimu”-NYUSI

“Tunaweza kusema kila kitu ila bila maisha yote tunayosema hayatoeleweka, JPM ni Rais mzuri, anashughulika na maisha ya Watanzania kutafuta nyumba nzuri, chakula, maji, afya na akiomba afya anataka ile afya ya Quality, hii ni zawadi Kwetu kuweka jiwe la msingi la Hospitali ya Rufaa Chato”-NYUSI