Rais wa zamani wa club ya Olympique Marseille ya Ufaransa Pape Diouf ,68, afariki dunia kutokana na maambukizi ya virusi vya corona. Diouf toka Jumamosi alikuwa amewekewa mashine maalum ya kusaidia mfumo wake wa upumuaji.

Mauti yamemkuta akiwa Dakar Senegal, familia yake ilitaka asafirishwe kutoka Senegal  akatibiwe Ufaransa lakini haikuwezekana kutokana na aina ya ugonjwa aliyokuwa anaumwa.