Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa Viongozi katika Taasisi zifuatazo:-

1. Kwa mujibu wa Uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 8(1) cha Sheria ya Uanzishwaji wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Namba 11 ya mwaka 2003, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua BALOZI MOHAMED RAMIA ABDIWAWA kuwa MWENYEKITI WA BODI YA UTUMISHI YA OFISI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI.

2. Kwa mujibu wa Uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 9(1) cha Sheria ya Chuo cha Utawala wa Umma Namba 1 ya 2007, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua DKT. MWINYI TALIB HAJI kuwa MKURUGENZI WA CHUO CHA UTAWALA WA UMMA(IPA), ZANZIBAR.

Uteuzi huo unaanzia tarehe 15 Mei, 2018.