Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) imemfungia maisha, Michael Richard Wambura kujishughulisha na masuala yote yanayohusiana na mpira wa miguu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilisema uamuzi wa kufungiwa kwa Wambura umetolewa juzi Januari 22 mwaka huu.

Kamati ya Nidhamu ya FIFA chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Anin Yeboah wa Ghana, imekazia hukumu ya Kamati ya Rufani ya Maadili ya TFF iliyotolewa Aprili 6, 2018,Hivyo.Adhabu hiyo imetolewa kutokana na Kamati ya Nidhamu ya FIFA kukazia hukumu ya Kamati ya Rufani ya Maadili ya TFF.

Wambura ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa TFF kuanzia juzi hatatakiwa kujishughulisha na masuala ya mpira wa miguu duniani kote.

TFF tayari imeshamkabidhi Wambura uamuzi huo,na inawakumbusha wana familia ya mpira wa miguu kuzingatia maadili na nidhamu kwa kufuata taratibu zake kwa mujibu wa Katiba za TFF, CAF na FIFA.