Mwili wa marehemu Bibi Cheka, unatarajiwa kuzikwa leo saa 10:00 jioni, nyumbani kwake eneo la Mnadani Bunju B, jijini Dar es salaam, ambapo kwa sasa mwili huo umehifadhiwa katika Hospitali ya Mloganzila.

Akizungumza leo Novemba 29, 2019 Mkubwa Fella, ambaye aliwahi kufanya naye kazi, amesema hawezi kuongea chochote kuhusu hilo ila yupo njiani kuelekea msibani maeneo ya Mnadani, Bunju B.

Kwa upande wake msanii Chege Chigunda, aliyewahi kuwa naye kwenye kundi moja amesema.

“Siwezi kuongelea msiba sana, kwa sisi waislamu kwetu sio nzuri kuongelea suala la misiba na kuvirusha kwenye vyombo vya habari” amesema Chege.

Jana Novemba 28, 2019, iliripotiwa kutokea kwa kifo cha msanii huyo, aliyefariki katika Hospitali ya Mloganzila na chanzo cha kifo chake kinadaiwa ni maradhi ya Moyo na presha.