Ratiba Mzee Majuto kuzikwa leo Tanga

Mwili wa muigizaji wa vichekesho Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ umewasili Donge nyumbani kwake jana 7.05 usiku .
 Safari ya kwenda Tanga kwa ajili ya mazishi ilianza saa 10.15 jioni baada ya kumuaga katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Leo Agosti 10,2018 kuanzia saa 5.45 mchana, ibada ya mazishi itafanyika katika msikiti wa Nuruguda uliopo karibu na nyumbani kwake na kuzikwa kijiji cha Kiruku yalipo mashamba yake nje kidogo ya jiji la Tanga.
Mzee Majuto alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya Tezi Dume ambapo Januari mwaka huu,alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam na kisha baadaye kupelekwa India kwa Matibabu zaidi . June 23, mwaka huu alirejea nchini na kupelekwa moja kwa moja katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alifariki dunia.