Ratiba ya usaili kwa walioomba nafasi za kazi katika Wizara mbali mbali za SMZ Pemba

Tume ya Utumishi Serikalini inawatangazia wale wote walioomba nafasi za kazi katika Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa upande wa Pemba wanatakiwa kufika kwenye usaili kwa mujibu wa Wizara walizoomba.

Wasailiwa wote wanatakiwa kuchukua vyeti vyao halisi vya kumalizia masomo, Cheti cha kuzaliwa pamoja na kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.

RATIBA YA USAILI

1. 17/11/2018 – USAILI UTAFANYIKA SKULI YA FIDEL CASTRO SAA 2:00 ASUBUHI
I. WIZARA YA UJENZI, MAWASILIANO NA USAFIRISHAJI – PEMBA
• Walinzi
• Fundi Welding
• Fundi Magari
II. OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ – PEMBA
• Ulinzi
• Dereva
• Wasafishaji Mji

2.18/11/2018 – USAILI UTAFANYIKA SKULI YA FIDEL CASTRO SAA 2:00 ASUBUHI
I. OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ – PEMBA
• Karani Masjala
• Afisa Utumishi
• Afisa Tehama
• Afisa Sheria
• Mtunza Ghala
• Afisa Manunuzi
• Muhandisi Ujenzi
• Afisa Mipango
• Afisa Habari na Uhusiano
• Afisa Uchumi
• Katibu Muhtasi
• Mwangalizi wa Ofisi

3. 19/11/2018 – USAILI UTAFANYIKA SKULI YA FIDEL CASTRO SAA 2:00 ASUBUHI
I. OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS – PEMBA
• Afisa Bioanuai (biodiversity/usimamizi wa Maliasili)
• Afisa Mabadiliko ya Tabia Nchi
• Mtunza Ghala
• Afisa Utumishi Msaidizi
• Mwangalizi wa Ofisi
• Msaidizi Afisa Manunuzi
• Katibu Muhtasi
• Karani Masjala
• Ulinzi
• Tarishi
• Afisa Sheria
• Dereva
• Wasaidizi Afisa Doria

4. 20/11/2018 – USAILI UTAFANYIKA SKULI YA FIDEL CASTRO SAA 2:00 ASUBUHI
I. WIZARA YA KILIMO, MALIASILI MIFUGO NA UVUVI – PEMBA
• Mwangalizi wa Ofisi
• Fundi Magari
• Msaidizi Fundi Magari
• Afisa Kilimo Msaidizi
• Afisa Mifugo
• Msaidizi Afisa Misitu
• Katibu Muhtasi
• Karani mapato
• Karani Diko
• Fundi Seremala
• Afisa Nyuki
• Afisa Kilimo
• Muuza Pembejeo
• Afisa Umwagiliaji

5. 21/11/2018 – USAILI UTAFANYIKA SKULI YA FIDEL CASTRO SAA 2:00 ASUBUHI

I. WIZARA YA KILIMO, MALIASILI MIFUGO NA UVUVI – PEMBA

• Ulinzi
• Dereva
• Muhudumu Shamba
• Afisa Mali za Serikali
• Mtunza Ghala