Staa wa muziki nchini Tanzania, Chui Rayvanny ambae ni mshindi wa Tuzo ya Bet 2017, amedokeza ujio wa Albamu yake mpya.

Kupitia ukurasa wa kijamii wa Instagram wa msanii huyu amebainisha kuachia Album, itakumbukwa kuwa mwaka huu Chui alitoa Extended Play (EP) yake inayokwenda kwa jina la “Flowers” ambayo ilikuwa na nyimbo sita.

Hivi karibuni imeelezwa kuwaRayvanny atafungua lebo yake, pia haijawekwa wazi ni lini hasa Album hiyo itatoka na jina lake ni lipi.