RC Kusini Unguja amtaka mkurugenzi halmashauri wilaya ya kati kuwa mbunifu

Mkurugenzi wa halmashauri wilayani ya Kati kwa kushiriki na wafanyakazi wake wametakiwa kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo ili kukuza mapato ya halmashaur hiyo.

Hayo yameelezwa na mkuu wa mkoa wa kusini Mh. Hassan Hatibu Hassan huko katika ukumbi wa halmashaur Dunga mjini Unguja.
Amesema katika kukuza mapato ya halmashauri hapana budi kubuni miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa viwanda, ukulima wa mbogamboga na mengineyo.
Amefahamisha kuwa endapo halmashuri hiyo itaanzisha bidhaa mbalimbali na kuzitafutia masoko ndani na nje ya nchi kupitia viwanda na kilimo zitaweza kukua kimapato na hata kukuza uchumi wa nchi na kufikia malengo yaliokusudiwa.
Akiendelea kuzungumza amesema kuwa Kuna baadhi ya mazao ambayo huweza kuzalishwa hapa visiwani ambavyo vinaviwango tofauti na mikoa mingine Kama vile vitunguu, tungule na hata matunda, hivyo ikiwekezwa kuwa ni mazao ya biashara wataweza kupiga hatua za mafanikio.
Aidha amewataka kuwasisitiza wafanyabiashara wa wilayani ya Kati kudumisha usafi wa mazingira kwani ni jukumu la watu wote.