Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema pamoja na matokeo ya jana bado najivunia ujasiri wao na kujituma kwa wachezaji wa Timu ya Taifa Stars.

RC Makonda amesema Taifa letu halijashindwa na Taifa Stars itaendelea kuwa nembo yetu huku akisema ipo siku tutainuka kwa nguvu kubwa kama tulivyoinuka baada ya miaka 39.

“Nimepata familia mpya tena isiyokata tamaa, Jeshi la kuaminika, Vijana wenye kiu na maono ya mbali. Leo wote tumewaona nao ni TAIFA STARS.”

“Pamoja na matokeo ya leo bado najivunia ujasiri wao na kujituma kwao. Watanzania Asanteni kwa kuiombea timu yetu na kuisukuma, kwa kuwatia MOYO wachezaji wetu na kuwaonesha wao ni wapambanaji halisi wa taifa letu, leo tumepoteza mchezo lakini Mungu wetu hajashindwa, Taifa letu halijashindwa na Taifa Stars itaendelea kuwa nembo yetu,” alisema Makonda.

“Ipo siku tutainuka kwa nguvu kubwa kama tulivyoinuka sasa baada ya miaka 39. Asante sana Mungu Kwa matokeo ya leo.Today we have lost the battle in the battle field, we have not lost the war! We are so much proud of our team!. Mungu ibariki Tanzania.”