Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, ameagiza kuwakata mishahara watumishi wote wa mkoa huo wanaodaiwa masurufi yaliyosababisha hoja ya kiukaguzi ya Sh milioni 4.7 katika ripoti ya Mdhibiti wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Agizo hilo alilitoa wakati wa kikao maalumu cha Baraza la Madiwani ya kupitia hoja ya mbalimbali  kutoka ripoti ya ukaguzi ya CAG kwa mwaka 2017/18.

Alisema ndani ya wiki watumishi wote wanaodaiwa wahakikishe wamelipa fedha hizo au wakatwe kwenye mishahara yao.

Mwanri alisema wasipo katwa fedha hizo hoja hiyo itaendelea kujitokeza na kuchafua hesabu za Manispaa ya Tabora.

Sanjari na hilo Mwanri huyo ametoa wiki mbilli kwa wakuu wa Idara kuhakikisha wamefanyia kazi hoja zote za CAG na kuwalisilisha vielelezo ili ziweze kufungwa.

Alisema watumishi ni vema wakajitahidi kuzuia hoja na zio kutoa maamuzi ambayo yanasababisha kuendelea kuzalisha hoja kila mwaka.