Ripoti iliyotolewa jana na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) na Shirika la Afya Duniani (WHO) imesema, mabilioni ya watu kote duniani walikosa huduma za maji, usafi na afya hadi mwaka 2017.

Ripoti pia inasema watu Bilioni 1.8 walipata maji safi ya kunywa tangu mwaka 2000, lakini bado kuna pengo kubwa la usawa katika upatikanaji wa huduma hizo, na kwamba asilimia 80 ya watu waishio vijijini wanakosa huduma hizo.