Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Ruby amefunguka kipaji cha Mwanamitindo, Hamisa Mobetto baada ya kuangukia kwenye muziki.

Ruby amesema kuwa Mwanamitindo huyo hana kipaji, kikubwa anachotakiwa kufanya ni kuhakikisha anawasikiliza waandishi wa nyimbo na kujua kwamba unaimba nini ili usiwakere watu kwenye masikio yao.

“Kusema ukweli ni kwamba Hamisa hana kipaji cha kusema huyu ana kipaji, kwahiyo watu tunaona na we know what is the talent isipokuwa kitu ambacho kinaweza kikamsaidia ni kujitahidi sana kusikiliza watu  walio mtangulia especially waandishi ok kuimba unaweza ukawa huna hiyo sauti lakini hakikisha unaimba nini kwa watu hakikisha unafikisha ujumbe ili mtu usimkere sana kwenye masikio yake, Ruby ameiambia Wasafi Tv.