Tunafahamu kuwa rushwa ni adui wa haki na inarejesha nyuma jitihada za maendeleo ya Taifa, hivyo basi tutumie nafasi zetu kuwa wazalendo kwa kusimamia na kuibua kero zinazohusiana na rushwa ili jamii iendelee kufahamu athari zinazoweza kujitokeza ikiwa tutaipa nafasi katika harakati zetu za maisha ya kila siku.