Leo Novemba 5, 2018 Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Kamati yake ya Maadili  limetangaza kumfungia maisha kutojihusisha na soka aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati yake ya Uchaguzi, Wakili Revocatus Kuuli kwa kukutwa na hatia ya kuweka hadharani nyaraka za shirikisho hilo na kuzisambaza kwa watu wasiohusika.

Awali kikao cha kamati ya Utendaji ya TFF kilimfikisha Kuuli mbele ya kamati ya maadili ambapo kamati hiyo imekuja na uamzi huo wa kumfungia maisha.

Kuuli ndiye alisimamia uchaguzi mkuu wa TFF Agosti 12, 2017, uchaguzi ambao ulifanyika jijini Dodoma na kumweka madarakani Rais wa sasa wa TFF Wallace Karia.