Baada ya ligi 5 bora barani Ulaya kumalizika kwa msimu 2018/19, wafungaji wa magoli wameongozwa na Lionel Messi, ambaye amechukua kiatu cha dhahabu nchini Hispania pamoja na Ulaya baada ya kufunga magoli 36 kwenye La Liga.

Wakati Messi akifunga mabao 36 ni mchezaji mwingine mmoja tu ambaye amefunga magoli zaidi ya 30, ambaye ni Kylian Mbappé wa Paris Saint-Germain, aliyefunga 33, huku washambuliaji wengine wakifunga kuanzia magoli 20 akiwemo Mbwana Samatta.

Kwa upande wa Ligi kuu ya Ubelgiji nahodha wa taifa Stars Mbwana Samatta, amefunga jumla ya magoli 23 hivyo kuwa amezidiwa na wachezaji watatu tu ambao ni Messi, Mbappe na Quagliarella huku akilingana na Duván Zapata.