Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametaka shule za kukuza vipaji kwa vijana ziwekwe katika hali nzuri ili kuweza kutayarisha wachezaji wazuri wa baadaye.

Pia amesema kilichofanyika jana ni Utanzania ambao umewakutanisha watu wa sehemu mbalimbali lakini wameweka kando tofauti zao ili kuhakikisha wanafanya vizuri kwa ajili ya taifa.

Ameyasema haya leo Jumatatu Machi 25, 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla iliyowakutanisha wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na bondia Hassan Mwakinyo.

Naomba sana muelewane muende kama Watanzania na makando kando mengine muyaweke pembeni ili muweze kufika mbali kwa sababu tayari mmeshatwikwa zigo jingine na sisi tutahakikisha tunatafuta namna ya kukuza vipaji vingi,” amesema Samia.

Pia amempongeza bondia Mwakinyo huku akiahidi Watanzania watamuundia kamati ili kuhakikisha kuwa mchezo wa ngumi unakua.

Mimi kama mama sina maneno mengi kwa sababu mnajua watu mkishinda ni furaha hivyo tunafurahia tu leo,” amesema Samia.