Imeelezwa kuwa changamoto ya uwepo wa saratani ya matiti kwa wanawake, imekuwa kichocheo kikubwa cha ndoa zao kuvunjika kwakuwa wanaume wengi hawana uelewa wa tatizo hilo.

Akizungumza mratibu wa Taasisi ya Saratani ya matiti nchini Kisa Mwakatobe, amesema kuwa licha ya uwepo wa changamoto hiyo bado kuna tatizo la gharama kubwa ya upatikanaji wa matiti bandia kwa wale waliotolewa matiti yao.

“Haya matiti bandia hayapatikani hapa nchini, mara nyingi tunayanunua China na Uingereza na ni bei ghali, yanauzwa dolla 50 hadi 95 kwa titi moja, kuna wanawake wengine tunawakuta wamejikataa wenyewe hali inayopelekea ndoa zao kuwa kwenye changamoto”, amesema Kisa Mwakatobe.

Ikumbukwe kuwa mwezi Oktoba ni mwezi wa kuadhimisha Saratani ya matiti Duniani, ambapo kampuni ya Coca-Cola Kwanza kupitia maji yake ya Dasani, imeaandaa matembezi ya hisani yenye lengo la kukusanya kiasi cha Shilingi milioni 100, kwa ajili ya kujenga mabweni ya kuwahifadhi wanawake kutoka mikoani wanaosubiri matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.