Seleman Matola ambaye ni Kocha wa Lipuli FC, amesema kuwa jeuri ya kikosi chake kuwa na mwendelezo wa kupata matokeo mazuri ni  sare waliyoipata na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu waliocheza uwanja wa Taifa.

Baada ya sare hiyo, Lipuli walifanikiwa kukusanya pointi 9 katika michezo ya Ligi kuu waliyocheza ambayo ni pamoja na Mbeya City kwa kuwachapa bao 2-0 wakiwa  ugenini, walishinda pia dhidi ya Ruvu Shooting uwanja wa Samora, Biashara United Samora  na kesho watakuwa nyumbani dhidi ya Ndanda SC.

Matola amesema kuwa vijana walipata kutambua uwezo walionao hasa baada ya kutoa sare na kikosi ambacho ni cha gharama kubwa tofauti na wao hali iliyowajenga kisaikolojia.

Mtola amesema “Kwa sasa Lipuli tupo vizuri baada ya kupata sare na Simba kuna nguvu mpya ambayo imeingia kwa wachezaji kwa sasa wanajiamini na kutumia uwezo wao wote wakiwa uwanjani hali inayosaidia kuweza kupata matokeo hivyo bado moto hauzimwi kwa sasa.

“Tumejipanga kufanya vizuri katika michezo yetu yote tutakayocheza kwa sasa hilo linawezekana kwani mpira ni mchezo ambao hauwezi kuficha matokeo yake yanapatikana uwanjani, mashabiki waendelee kutupa sapoti,”.